Psalms 52

Hukumu Ya Mungu

(Kwa Mwimbishaji: Utenzi Wa Daudi. Baada Ya Doegi, Mwedomu, Kumwendea Sauli Na Kumjulisha Kuwa Daudi Amekwenda Nyumbani Kwa Ahimeleki)


1 aEwe jitu, mbona unajivunia ubaya?
Kwa nini unajivuna mchana kutwa,
wewe ambaye ni fedheha mbele za Mungu?

2 bUlimi wako hupanga mashauri mabaya ya maangamizi.
Ni kama wembe mkali, ninyi mfanyao hila.

3 cUnapenda mabaya kuliko mema,
uongo kuliko kusema kweli.

4 dUnapenda kila neno lenye kudhuru,
ewe ulimi wenye hila!


5 eHakika Mungu atakushusha chini
kwa maangamizi ya milele:
atakunyakua na kukuondoa kwa nguvu
kutoka hema yako,
atakung’oa kutoka nchi ya walio hai.

6 fWenye haki wataona na kuogopa,
watamcheka, wakisema,

7 g“Huyu ni yule mtu ambaye
hakumfanya Mungu kuwa ngome yake,
bali alitumainia wingi wa utajiri wake,
na akawa hodari kwa kuwaangamiza wengine!”

Neema Ya Mungu


8 hLakini mimi ni kama mti wa mzeituni
unaostawi katika nyumba ya Mungu,
nautegemea upendo wa Mungu usiokoma
milele na milele.

9 iNitakusifu milele kwa yale uliyoyatenda,
nitatumaini jina lako, kwa kuwa jina lako ni jema.
Nitakusifu mbele ya watakatifu wako.
Copyright information for SwhKC